| Jinsi ya kuomba kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2010
Sauti za Busara ni tamasha la muziki la kimataifa,ambalo hufanyika kila mwezi wa pili Zanzibar,kuonyesha muziki kutoka sehemu zinazo zungumza kiswahili, katika bara la Afrika na pande zote .
Miaka iliyopita ,zaidi ya vikundi 240 vimekwisha shiriki baadhi yao ni Jose Chameleone, Juma Nature na Wanaume Family TMK, Samba Mapangala, Saida Karoli, Natacha Atlas, Didier Awadi, Eric Wainaina, Bassekou Kouyate, Seckou Keita Quartet, Culture Musical Club na wengineo wengi.
MWISHO wa kupokea maombi |
| Kimataifa 31 July 2009 |
Tanzania
31 August 2009 |
Kwa wasanii watakao shiriki katika tamasha, kwa kawaida hulipwa pesa kwa ajiri ya onyesho na matumizi yao wakiwa Zanzibar, ikiwa ni usafiri , malazi,chakula na matumizi madogo madogo.Kwa wasanii kutoka nje kawaida wanatakiwa kutafuta wadhamini wao wenyewe kwa ajili ya usafiri
Jopo la uchaguzi litakutana mwanzoni mwa mwezi wa nane kuchagua wasanii watakao shiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2010. Wasanii wote watajulishwa maamuzi ya jopo kwa kupitia barua pepe mnamo mwezi tisa
Maombi yako yatashughulikiwa endapo tutapokea maombi kutoka kwako kabla ya MWISHO wa kutuma maombi. Maombi yako lazima yaambatanishwe na vitu vifuatavyo:
- form ya maombi iliyojazwa na maelezo mafupi (maneno yasizidi 1000)
- nakala moja au mbili ya kazi zako (CD, DVD, au MP3)
- picha moja au mbili( JPG au karatasi)
Tafadhali tuma nakala,picha na maelezo kupitia anwani yetu ya ofisini kama inavyoonekana hapo chini.
(Form inaweza kujazwa kupitia mtandao wa intenate) |
Tafadhali jaza form.Unaweza kujaza kupitia mtandao wa intenate,au chapisha na tuma kupitia sanduku la posta hapo chini.
* Jaza kama inavyotakiwa
This form is also available in ENGLISH. Please choose
before starting to fill in the details.
Ce formulaire est également disponsible en FRANÇAIS. Veuillez faire votre choix avant de commencer à compléter.
|