Do not reply to this email address. If you would like to get in touch please use busara@zanlink.com
Usijibu kutumia barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@zanlink.com

Busara symbol - click for home page

BUSARA NEWSLETTER

November 2009

In this edition:
SzB logo
>>> English version

Sauti za Busara 2010

topback to the top

Mtanange wa saba wa tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika Zanzibar kila mwaka itakuwa ni kuanzia tarehe 11 hadi 16 Februari 2010; hakutakuwa na kiingilio kwa watakaoingia kabla ya saa kumi na moja.

Sauti za Busara ni tamasha la kimataifa ambalo linautambulisha na kuutangaza muziki wa Afrika Mashariki, na ambalo hufanyika katika kila wiki ya pili ya mwezi wa Februari kila mwaka kisiwani Zanzibar.

2010 fROOTS line-up advert

Wasanii watakaoshiriki 2010

topback to the top

Wasanii waliohakikisha

(angalia 10 bora hapa)

Thandiswa (South Africa) > Fresh Jumbe & African Express (Tanzania / Japan) > Simba & Brown Band (Mozambique) > Isaac Blackman & The Love Circle (Trinidad & Tobago) > Nyota Ndogo (Kenya) > Jimmy Omonga (DRC / NL) > Jhikoman (Tanzania) > Mzungu Kichaa (Denmark / Tanzania) > Tunda Man (Tanzania) > Makadem (Kenya) > Ikwani Safaa Musical Club ft Tamalyn Dallal (Zanzibar / USA) > Del & Diho (Mayotte) > Obibase (Guinea) > Mari Boine (Norway) > Dawda Jobarteh (The Gambia) > Sousou & Maher Cissoko (Senegal / Sweden) > Xova (UK) > Massar Egbari (Egypt) > Debo  Band (Ethiopia / USA) > Bamba Nazar & The Pilgrimage (Suriname / NL) > Joel Sebunjo & Sundiata (Uganda) > Juliana Kanyomozi (Uganda) > Maureen Lupo Lilanda (Zambia) > Nass Makan (Egypt) > Tausi Women's Taarab (Zanzibar) > Mim Suleiman (Zanzibar / UK) > Kunja Dance Theatre (Kenya) > Swifatui Abraar Group (Tanzania) > DJ Eddy (Zanzibar) > DJ Yusuf (UK / Zanzibar) > Sowers Group (Tanzania) > Best of WaPi (Tanzania) > Sosolya Dance Academy (Uganda) > Mapacha Africa (Kenya) > Sinachuki Kidumbak (Zanzibar) > Shirikisho Sanaa (Zanzibar) > Tunaweza Band (Tanzania) > KVZ Tupendane (Pemba) > Keita & Swahili Vibes (Zanzibar) > Maia Von Lekow (Kenya) na wengineo.

Asilimia mia moja itakuwa live ( hakuna kuimba na CD)!

(watakuwa katika tovuti na mwengineo  watatangazwa)

Thandiswa (South Africa)

Thandiswa (South Africa)

 
Joel Sebunjo & Sundiata (Uganda)

Joel Sebunjo (Uganda)

Tiketi na viingilio

topback to the top

Likionyesha wasanii maarufu na wanaochipukia na waliofanyiwa uteuzi makini zaidi ya 400 (vikundi 40 kwa jumla), Sauti za Busara imeweza kuthibitisha kuwa ni tukio kubwa na bora zaidi la muziki hapa Afrika mashariki, ni tukio linalowaunganisha watu katika mazingira ya kusherehekea.

Muziki kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa saba usiku Alhamisi mpaka Jumapili.

Kiingilio ni bure kwa wale watakao ingia kabla ya saa kumi na moja jioni. Baada ya hapo utahitajika kuwa na tiketi au pasi maalum ya kuingilia. Bei zinatofautiana baina ya wageni, wakaazi na. Kwa wanaopendelea kukaa kwenye viti kuna tiketi maalum za VIP.

Usafiri Na Malazi

topback to the top

Kwa mahitaji yako yote ya usafiri na malazi hapa Zanzibar pamoja na usafiri wa anga kwa Afrika, tunafurahi kukufahamisha kuwa wasiliana na Tabasam Tours iliyopo Zanzibar. Wao wanatoa huduma za uhakika za usafiri wa kwenda na kurudi uwanja wa ndege, maandalizi ya malazi na pia unaweza kupata pasi ya siku nne ya tamasha kupitia kwao.

Na zaidi ni kwamba kutakuwa na punguzo la asilimia 5 kwa wale watakaowatumia Tabasam Tours kufanya taratibu zao za malazi. Ulizia "Busara Discount".

Usafiri Na Malazi>>>

More Opportunities

topback to the top

Busara Xtra

Kumbuka kuwa, siyo sisi pekee. Zanzibar ina maeneo mengine mengi ambako matukio kedekede hufanyika kwa mfano katika mahoteli, migahawa na kumbi mbalimbalii. Hii tumeibatiza jina la “Busara Xtra” na tutafanya kila jitihada kukufahamisha yale yote yatakayojiri.

Tuambie habari yako kama unaonyesho mahali popote tutatangaza bure!

Vibanda

Ni nafasi chache za vibanda zimebaki kwa ajili ya biashara. Kwa maelezo zaidi tembelea hapa.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 1 Disemba 2009

Matangazo

Nafasi za matangazo ni chache, kuweka tangazo la shughuli yako katika programu ya tamasha ni njia bora ya kuonyesha kutuunga mkono katika tukio hili adhimu.

Mwisho wa kupokea matangazo ni tarehe 11 Disemba 2009

Udhamini

Tamasha hili litawezekana tu kutokana na ufadhili na udhamini mkubwa wa hali na mali kutoka katika vyanzo mbalimbali. Kwa wafadhili na wadhamini mbalimbali wenye nia ya kushirikiana nasi kulifanikisha, tumeandaa maelekezo yanayoainisha utaratibu mzima. Tunazo njia mbalimbali za kulionyesha jina lako kuwa ni mmoja wa wale waliolifanikisha Tamasha. Iwapo una nia  hiyo tafadhali wasiliana nasi

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 1 Disemba 2009

Mashindano

topback to the top

Zanzibar festival classics CD Busara Book: First Five Years
Busara t-shirts

Shinda!

kitabu cha Busara

Filamu ya Tamasha

Pasi ya kuingilia katika tamasha

na fulana

Tutatoa zawadi za Christmas kwa watu watatu waliojiunga katika orodha yetu ya habari ambao watamalizia kujaza sentensi ifuatayo:

"Kuona muziki wa Kiafrika unapigwa live Afrika ni vizuri kwa sababu…"

Tutumie jibu lako kwa njia ya barua pepe kabla ya tarehe 1 Disemba katika busara@zanlink.com

Usisahau kutuambia anuani yako ya posta na size yako ya fulana  kama ni (S/M/L/XL/XXL)

Bi Kidude - DVD

topback to the top

AS OLD AS MY TONGUE
The myth and life of Bi Kidude

Unaweza kununua FILAMU hii kutoka kampuni ya Sterns Music (Uingereza) na watakutumia kwa njia ya posta popote pale ulipo duniani.

Maelezo zaidi kuhusu filamu yanapatikana kupitia
asoldasmytongue.net

“Impressive and engrossing” Charlie Gillett
“A remarkable documentary” Simon Broughton, Songlines
“A delight from beginning to end” Howard Male, The Independent
“A living folk-memory of Swahili music” Peter Bradshaw, The Guardian

Bi Kidude film postcard

 

Sauti za Busara 2010 Imewezeshwa Na

topback to the top

Waandaaji wa tamasha wanapenda kushukuru imani, busara, maono na msaada mkubwa wa wafadhili na wadhamini, ambao kama si wao Sauti za Busara lisingewezeka. Katika kipindi hiki cha maandalizi, bajeti na mipango inatupa wakati mgumu sana. Tumepatiwa ahadi kadha wa kadha na bado tunahitaji misaada zaidi. Hadi hivi sasa, tamasha limewezeshwa na:


principal sponsor

Zantel logo

main sponsors

HIVOS - people unlimited
Norwegian Embassy
British Council

logo sponsors

<< YOUR LOGO COULD BE HERE >>

media sponsors

fROOTS
ZG Design

festival party sponsor

<< YOUR LOGO COULD BE HERE >>

Goethe-Institut, US Embassy, UNDP, Gallery Tours, ZanAir, Memories of Zanzibar, Zanlink, Dhow Countries Music Academy , WOMEX, Embassy of Denmark, Stone Town Café, Mercury’s Restaurant, Archipelago Café & Restaurant, Tabasam Tours, Monsoon Restaurant, Linear Velocity, Footcandles, www.zanzibar.net

Thanks also to: Ministry for Information, Culture & Sports, and to all the people of Zanzibar:
"Shukurani kwa kukubali kuwa tamasha hili ni letu sote na mchango wenu ndio ambao umelifanikisha."

Contact Us

topback to the top

Busara Promotions logo

www.busaramusic.org

Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Find us between Africa House and Serena Inn, opposite Amore Mio. 

busara@zanlink.com

Tel: +255 24 223 2423
or +255 784 925 499
or +255 773 822 294


Tafadhali tuma habari hii kwa marafiki wote wapenzi wa muziki. Kujiunga au kujitoa katika orodha yetu ya habari ni rahisi
andika anuani yako ya barua pepe kwenye kisanduku kilichopo katika tovuti yetu ambayo ni www.busaramusic.org